Frenkie de Jong Aendelea Kusisitiza Bado yupo sana Barca

Kiungo wa klabu ya Fc Barcelona na timu ya taifa ya Uholanzi Frenkie de Jong ameendelea kusisitiza kua mipango yake ni kubaki ndani ya klabu ya Barcelona kwa muda mrefu zaidi.

Kiungo Frenkie de Jong amesema anatarajia kubaki ndani ya klabu ya Barcelona kwa muda mrefu zaidi na anataka kusalia klabuni hapo na kucheza katika dimba lipya la Camp nou, Klabu ya Barcelona ipo kwenye mpango kufanya marekebisho katika uwanja wake wasasa.frenkie de jongKiungo huyo wa kimataifa wa Uholanzi amekua kwenye kiwango bora sana ndani ya klabu hiyo msimu huu, Huku akiwa moja ya wachezaji wa kutumainiwa na muhimu kwa klabu hiyo chini ya kocha Xavi Hernandez na hiyo imekuja baada ya kuimarika kwa kiungo huyo zaidi msimu huu.

Frenkie de Jong ni kama ameikata maini klabu ya Manchester United ambayo imekua ikimfuatilia kwa muda mrefu mchezaji huyo, Kwani kiungo huyo amesema haoni akiondoka ndani ya klabu ya Barcelona kwani klabuu hiyo ni klabu ya ndoto yake zake na anafurahi kuwepo hapo.frenkie de jongKlabu ya Manchester United inaelezwa licha ya kauli za Frenkie de Jong lakini bado imepanga kumhitaji tena kwenye dirisha kubw ala usajili majira ya joto mwezi wa sita na wameandaa ofa kubwa kwa klabu hiyo, Hivo kinachosubiriwa ni kama klabu ya Barcelona kama itavutiwa na ofa ambayo imeekwa na Man United.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.