Napoli vs Ac Milan Vita ya Ndugu

Klabu ya Napoli na Ac Milan watakutana katika hatua ya robo fainali ya ligi ya mabingwa ulaya baada ya droo kuchezeshwa leo na kuwakutanisha miamba hiyo kutoka nchini Italia katika michuano hiyo mikubwa barani Ulaya.

Napoli watakutana na ndugu zao klabu ya Ac Milan katika hatua ya robo fainali ya ligi ya mabingwa ulaya kulikua kuna hatari ya timu kutoka Italia kukutana katika hatua hii ya robo fainali, Kwani klabu tatu kutoka nchini Italia zilifanikiwa kutinga hatua ya robo fainali ya michuano hiyo.napoliBaada ya vilabu hivo viwili kukutana katika hatua ya robo fainali ya ligi ya mabingwa ulaya imekua kama utabiri kutimia kwa watu wengi ambao walitabiri huenda timu za Italia zingekutana katika hatua hii, Hicho ndio kilichotokea kwani droo iliyochezeshwa leo imekutanisha timu za Italia katika hatua ya robo fainali.

Napoli ambao wako kwenye msimu bora kabisa msimu huu wakiwa wamefuzu hatua ya robo fainali ya ligi ya mabingwa ulaya kwa mara ya kwanza wanaenda kukutana na ndugu zao Ac Milan ambao hawana msimu bora sana, Lakini Ac Milan wako ni klabu ambayo ina historia nzuri na uzoefu wa michuano hiyo.napoliVita hii ya ndugu kwenye ligi ya mabingwa ulaya inasubiriwa kwa hamu kubwa huku klabu ya Napoli ikipewa nafasi kubwa ya kusonga mbele kwenye pambano hilo kutokana na ubora wake msimu huu, Lakini uzoefu wa Ac Milan kwenye michuano hiyo unaweza pia kua kikwazo cha vijana wa Luciano Spalletti.

 

Acha ujumbe