Pogba Akumbwa na Tuhuma nzito

Kiungo wa klabu ya Juventus na timu ya taifa ya Ufaransa Paul Pogba anakabiliwa na tuhuma nzito ya kutumia madawa ya kuongeza nguvu mchezoni jambo ambalo ni katazo kubwa.

Kiungo huyo inaelezwa aligundulika alipofanyiwa vipimo katika mchezo dhidi ya Udinese tarehe 20 mwezi wa nane, Hivo kinachosubiriwa kwasasa ni taarifa kutoka kwa klabu yake ya Juventus.pogbaVyanzo mbalimbali kutoka nchini Italia vinaeleza klabu ya Juventus ndio inasubiriwa kutoa tamko kwasasa ili kuthibitisha habari hizi na kiungo Paul Pogba kujua hatma yake ndani ya klabu hiyo.

Inafahamika wachezaji wakigundulika wametumia dawa za kuongeza nguvu mchezoni hua wanafungiwa kwa kipindi fulani kutojihusisha na mpira wa miguu na hii imeshawahi kuwakumba wachezaji kadhaa barani ulaya kama Kolo Toure, Andre Onana, na Diego Maradona.pogbaKutokana na jambo hili inaendelea kuaminisha wadau wengi wa mpira wa miguu kua unaweza kua mwisho wa kiungo Paul Pogba, Kwani kiungo huyo amekua hana muendelezo mzuri kipindi cha hivi karibuni na hiyo ni kutokana na majeraha na sasa anakumbana shutuma hizi hali inazidi kua mbaya zaidi.

Acha ujumbe