Pogba Afungiwa Rasmi

Kiungo Paul Pogba ambaye anakabiliwa na mashataka ya kujihusisha na matumizi ya dawa za kuongeza nguvu mchezoni hatimae amefungiwa na kujihusisha shughuli za kimpira.

Shirikisho la kupinga matumizi ya dawa za kuongeza nguvu mchezoni nchini Italia imemfungia kiungo Paul Pogba kujihusisha na mpira wa miguu kwa muda ambao haujawekwa wazi baada ya kiungo huyo kubainika.pogbaKiungo huyo raia wa kimataifa wa Ufaransa alibainika kua kwenye utumizi wa madawa ya kuongeza nguvu mchezoni katika mchezo wa ligi kuu ya Italia uliopigwa tarehe 20 mwezi wa nane dhidi ya klabu ya Udinese.

Klabu ya Juventus mpaka sasa haijatoa taarifa yeyote juu ya kiungo wao huyo juu ya tuhuma hizo zilizothibitishwa na mamlaka, Lakini vyanzo kutoka nchini Italia vimeeleza kua klabu hiyo iko kwenye mchakato wa kuachia taarifa rasmi.pogbaKiungo Paul Pogba amekua kwenye kipindi kigumu kwa muda wa takribani mwaka mmoja sasa, Kwani msimu uliomalizika karibia wote alikua anaandamwa na majeraha na msimu huu amekumbana na tuhuma za matumzi ya dawa za kuongeza nguvu mchezoni.

Acha ujumbe