MSHAMBULIAJI wa klabu ya Manchester United, Cristiano Ronaldo, ameomba radhi baada ya kuonekana kurusha simu ya shabiki wake chini na kuivunja kufuatia kipigo cha timu yake dhidi ya Everton.

Picha mbalimbali zimeonyesha Ronaldo akishusha mkono wake wa kulia kuelekea ardhini kabla ya simu inayoonekana kugongana na kuruka juu, alipokuwa akitoka nje ya uwanja kufuatia kipigo cha 1-0 kwenye dimba la Goodison Park.

 

ronaldo, Ronaldo Aomba Radhi kwa Kuvunja Simu ya Shabiki., Meridianbet

United wamekiri kuona tukio hilo linalosambazwa kwa kasi katika mitandao ya kijamii kufuatia mchezo huo, na klabu ilisema Jumamosi mchana walikuwa wakichunguza tukio hilo.

Ronaldo ameandika katika mtandao wake wa Instagram na kuomba radhi kwa tukio hilo: “Si rahisi kushughulika na mihemko katika nyakati ngumu kama zile tunazokabiliana nazo. Hata hivyo, siku zote tunapaswa kuwa na heshima, subira na kuweka mfano kwa vijana wote wanaopenda mchezo huo mzuri.

 

“Ningependa kuomba radhi kwa hasira yangu na, ikiwezekana, ningependa kumwalika shabiki huyu kutazama mchezo ujao hapa Old Trafford kama ishara ya mchezo wa haki na wa kimichezo.”

Ilikuwa siku mbaya uwanjani kwa Ronaldo na Manchester United huku bao la Anthony Gordon la kipindi cha kwanza likiwapa wenyeji Everton pointi tatu muhimu.

United wameshinda mchezo moja pekee katika mechi tano za Ligi kuu ya Uingereza, sasa wanaonekana kutokuwa na uwezekano wa kufuzu kwa Ligi ya Mabingwa msimu ujao.


VUNA MKWANJA NA AVIATOR

Maana halisi ya ushindi mkubwa unaipata katika kasino ya mtandaoni ya Aviator kutoka meridianbettz. Andaa kapu la ushindi wa mkwanja na beti kibao za BUREEE.

 

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

SOMA ZAIDI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa