Umri ni namba tu. Uwezo wake uwanjani sio kitu cha kutilia mashaka. Cristiano Ronaldo ametwaa tuzo ya pili mfululizo ya mchezaji bora wa mwezi Manchester United.

Baada ya kutwaa tuzo hiyo mwezi Machi, Ronaldo ameondoka tena na tuzo hiyo mwezi April baada ya kuwa miongoni mwa (kama sio mchezaji pekee) wachezaji waliofanya vizuri uwanjani ndani ya Manchester United.

Katika michezo 4 ya United kwa mwezi April, CR7 amepachika magoli 5. Ndiye mchezaji pekee aliyeonesha uwezo wa kufanya maajabu uwanjani hata katika nyakati ngumu za ndani na nje ya uwanja.

Ronaldo, Ronaldo Mchezaji Bora Wa Mwezi, Meridianbet
CR7 baada ya kufunga goli dhidi ya Arsenal, 2022.

Aliukosa mchezo dhidi ya Liverpool baada ya kupata msiba wa mtoto wake lakini, alirejea uwanjani mapema kuliko ilivyodhaniwa na kuendelea kuisaidia United kama vile hakuna kitu kimempata, huu ni ukomavu mkubwa wa akili.

Miongoni mwa magoli aliyofunga, goli lake dhidi ya Arsenal lilikua ni goli lake la 100 kwenye EPL na hii inamfanya Ronaldo kuwa miongoni mwa wachezaji wachache waliofunga idadi hiyo ya magoli kwenye ligi 2 tofauti (alishafanya hivyo alipokuwa Real Madrid).

Wastani wa kura 74% za mashabiki wa United, unamtoa Cristiano kimasomaso na kuwazidi David DeGea (21%) na Nemanja Matic (5%) kwenye kinyang’anyiro hiko.


TENGENEZA FAIDA NA ZEUS ANCIENT FORTUNES

Una Kila sababu ya kufurahia wiki yako na kutengeneza mwaka huu uwe wa faida zaidi katika kasino zetu za mtandaoni za meridianbettz. Mchezo wa Zeus Ancient Fortunes unakuongoza kutekeleza hilo.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa