Lionel Messi anapitia wakati mgumu zaidi maishani mwake. Mabao tisa msimu mzima. Tuweke takwimu sawa! Msimu uliondoka aliweka kambani mabao 38.

Ni kweli Messi ameisha?? Labda swali zuri ni umewahi kusikia wazungu wakisema Lionel Messi ameisha?

Chama
Chama

Wanajua anapitia nyakati ngumu na hazitadumu. Kwa yale aliyofanya wana hakika huyu si Messi bali ni nyakati tu.

Ni kwamba tu jina la Lionel Messi ni rahisi zaidi kulitumia kuuza habari. Ni jina zuri linaloweza kuuza taarifa yako ikatembea.

Ndiyo maana purukushani zinakuwa nyingi Messi anapofanya vibaya au vizuri . Benzema akifunga hat-trick ni stori lakini Messi akipiga hat-trick ni stori ya kusisimua.

Leo Robert Lewandowski akose penalt ni stori, lakini Lionel Messi akose penalt ni story ya kusisimua. Hakukosea Fid Q!

Messi wanajua hajaisha lakini wanatumia tu jina lake kuuza habari. Jina la Messi kuwa katika nyakati ngumu linavutia zaidi kuliko likiwa katika nyakati nzuri.

Rejea tena Ronaldo alivoanza maisha yake Juve. Juve waliishia robo fainali ya UEFA lakini mzigo ulitishwa kwa Ronaldo. Walifeli Juve au alifeli Ronaldo??

Dunia inapenda upande mweusi zaidi wa mtu anayefanya vizuri zaidi katika eneo lake. Dunia inafurahia zaidi upande wa giza kuliko nuru.

Chama
Chama
Nikuulize tena Chama ameisha?? Baada ya kuwa kiungo bora wa ligi, ndani ya miezi nane tu tunaweza kusema Chama ameisha kisa amerudi nchini??

Tazama takwimu zake kisha kumbuka muda ambao hakuwa uwanjani kisha nikuulize tena Chama ameisha??

Chama hajui kucheza mechi za derby??


TENGENEZA FAIDA NA ZEUS ANCIENT FORTUNES

Una Kila sababu ya kufurahia wiki yako na kutengeneza mwaka huu uwe wa faida zaidi katika kasino zetu za mtandaoni za meridianbettz. Mchezo wa Zeus Ancient Fortunes unakuongoza kutekeleza hilo.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa