Sean Dyche Atimuliwa Burnley Baada ya Miaka 10.

 

Meneja wa Burnley, Sean Dyche amefukuzwa kazi katika klabu hiyo baada ya miaka 10 wakati timu hiyo ikipambana na kushuka daraja kutoka katika Ligi ya EPL.

 

Burnley kwa sasa wako nafasi ya 18 kwenye jedwali, pointi nne kutoka nafasi ya 17. Wameshinda mchezo mmoja tu kati ya saba iliyopita wakifungwa 2-0 Norwich siku ya Jumapili.

“Klabu ya soka ya Burnley inathibitisha kuwa imeachana na meneja Sean Dyche, meneja msaidizi Ian Woan, kocha wa kikosi cha kwanza Steve Stone na kocha wa makipa Billy Mercer.” iliandika taarifa katika mtandao wa Twitter wa klabu hiyo.

Kocha wa U23s Mike Jackson, akisaidiwa na mkurugenzi wa akademi Paul Jenkins, kocha wa makipa wa U23s Connor King na nahodha wa klabu Ben Mee wameombwa kuchukua jukumu la kuinoa timu hiyo kwa mchezo wa Jumapili dhidi ya West Ham.

Kocha huyo mwenye umri wa miaka 50 aliiongoza Burnley kupandishwa daraja mara mbili kutoka kwa Championship, mara ya mwisho msimu wa 2015/16.

Sean Dyche anakuwa meneja aliyekaa muda mrefu zaidi katika ligi ya Premier, baada ya kuteuliwa kuwa meneja wa Burnley mnamo Oktoba 2012. Meneja anaefwata kukaa muda mrefu zaidi katika kitengo hicho ni Jürgen Klopp wa Liverpool (miaka 6 na siku 189).


VUNA MKWANJA NA AVIATOR

Maana halisi ya ushindi mkubwa unaipata katika kasino ya mtandaoni ya Aviator kutoka meridianbettz. Andaa kapu la ushindi wa mkwanja na beti kibao za BUREEE.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

SOMA ZAIDI

Acha ujumbe