Mapema wiki hii, kulikua na taarifa mitandaoni kuhusu baadhi ya mashabiki wa Manchester United kufanya maandamano wiki hii. Kazi imeanza.

Baadhi ya mashabiki wa Man United wamejitokeza kwenye maandamano ya amani kwenye uwanja wa mazoezi (Carrington Complex) leo wakati timu hiyo ikiwa inajiandaa na mchezo dhidi ya Norwich City wikiendi hii.

Maandamano haya yanalenga kuendelea kushinikiza umiliki wa United (Familia ya Glazers) kuachia timu hiyo ambayo wamekuwa wakiimiliki toka 2005. Mwaka jana, kwenye mchezo dhidi ya Liverpool, kulitokea hali kama hii na mchezo ulighairishwa.

mashabiki, Mashabiki Wameanzia Carrington., Meridianbet
Baadhi ya mashabiki wa Man United wakiwa na mabango yenye jumbe za kuitaka familia ya Glazers kuachia umiliki wa klabu hiyo.

Safari hii, idara ya ulinzi na usalama imehakikisha waandamanaji hao hawana nafasi ya kuingia kwenye uwanja huo kama ilivyokuwa mwaka jana. Badala yake, maafisa wa polisi walihitajika ili kuimarisha ulinzi na kuwatawanya mashabiki wao kwa amani na utulivu.

Hata hivyo, taarifa rasmi kutoka United zimethibitisha uwepo wa waandamaji hao na pia, umesisitiza kuheshimu mawazo yao (waandamanaji) na kama klabu, itaendelea kuwakaribu na mashabiki wake.


VUNA MKWANJA NA AVIATOR

Maana halisi ya ushindi mkubwa unaipata katika kasino ya mtandaoni ya Aviator kutoka meridianbettz. Andaa kapu la ushindi wa mkwanja na beti kibao za BUREEE.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

SOMA ZAIDI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa