Kasi ya fununu za Erik Ten Hag na Manchester United inaongezeka. Ukilisikia jina lake kwa harakaharaka unawezadhani tayari ameshapewa timu kumbe bado ni kocha wa Ajax.

Japokuwa mwenyewe anakwepa kutoa neno kuhusu Man United, inaaminika, mchongo wa kumkabidhi timu Ten Hag umekamilika kwa asilimia 90% na sasa ni suala la muda tu. Pengine wiki ijayo itatoa picha halisi baada ya mchezo wa fainali dhidi ya PSV.

Erik anajulikana kwa kuongoza timu inayojengwa na vijana wenye ari na uchu wa kujituma na kuipambania timu kwa kila hali. Kwa kikosi cha Man United ya sasa, hii hatoipata kwa wachezaji wote, ni wachache sana wenye sifa hizi.

Umri na mfumo wa maisha ya mchezaji (ndani na nje ya uwanja) pia ni kitu kingine ambacho kocha huyu anakizingatia zaidi. Katika hili, Cristiano Ronaldo ni muhanga wa uteuzi wa kocha huyu. Inasemekana, Ten Hag ameshawaambia vigogo wa United kuwa CR7 sio mchezaji wa kariba yake ya uchezaji na, hayupo kwenye mipango yake ya muda mrefu.

Ten Hag, Ten Hag Afungua Milango Kwa CR7, Meridianbet

CR7 toka amerejea United, hajawa kwenye ubora wake na alichokikuta pengine sio alichokitarajia Old Trafford. Japokuwa kulikua na fununu kuwa anafikiria kuondoka mwishoni mwa msimu huu, huenda ujio wa Erik na mipango yake kuanzia mwezi Juni, 2022 itaongezea cheche kwenye mchakato wa kuondoka kwa Cristiano Ronaldo.

Ama hakika, milango ya kuondokea Old Trafford ipo wazi kwa CR7 na wachezaji wengine wengi.


VUNA MKWANJA NA AVIATOR

Maana halisi ya ushindi mkubwa unaipata katika kasino ya mtandaoni ya Aviator kutoka meridianbettz. Andaa kapu la ushindi wa mkwanja na beti kibao za BUREEE.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

SOMA ZAIDI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa