Senzo Aingilia Kati Sakata la Uwekezaji wa GSM.

 

Kaimu Mtendaji Mkuu wa Yanga SC, Senzo Mazingisa amewakemea wanahabari walioanzisha mijadala yenye lengo la kuwakatisha tamaa wawekezaji wanaojitoa kukuza soka la Tanzania, GSM ikiwa imelengwa zaidi.

Aidha Senzo amezitaka Mamlaka za usimamizi wa soka nchini kutokalia kimya mijadala hiyo iliyoanzishwa kwa malengo maovu. Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii, Senzo ametoa maoni yake kuhusu mijadala hiyo;

 

Senzo mbatha

“Ni kwa masikitiko makubwa kwamba tunasoma mijadala inayomshambulia Mfadhili wetu na mdhamini wetu bila sababu za msingi”

“Mtazamo ambao unaonyeshwa na wafanyakazi wengi wa vyombo vya habari na watu binafsi kuelekea watu wenye sifa nzuri wanaoleta pesa kwenye soka lazima ulaaniwe”

“Haiwezekani kuwa katika nyakati hizi za majaribu ambapo wafadhili hawajitoi sana kudhamini soka na tuna watu binafsi wanaoshambulia watu wale wale ambao wanatumia pesa zao kusaidia soka”

“Je, ni kwa sababu Yanga imeimarika na kufanya vizuri chini ya ufadhili wa GSM ndiyo maana watu wanaona kuna haja ya kumshambulia mfadhili wetu?”

“Natahadharisha ujinga huu na kushauri kwamba ushughulikiwe mara moja na vyombo vinavyohusika na michezo. Kuna ubaya gani kwa GSM kusaidia vilabu vingine vinavyohitaji usaidizi?”

“Hoja wanazotoa ni dhaifu sana zenye lengo la kuleta usumbufu na hofu kwa GSM. Mdhamini wetu endelea na kazi hiyo nzuri na tuendelee kuunga mkono GSM. Kama Yanga, tunashukuru kwa msaada wako wa kifedha kwa klabu”

“Kinachoendelea ni dalili kuwa brand ya GSM inakua na inawasumbua wengine huko sokoni naomba watu waiunge mkono GSM kwa uwekezaji kwenye soka ambayo ni moja ya nguzo muhimu za kijamii katika ustawi wa Tanzania” aliongeza.


NJIA RAHISI YA MKWANJA NA TITAN DICE

Unawezaje kuikosa hii! njia rahisi ya kutengeneza mkwanja katika kasino maridhawa za meridianbet. Muda wa kufurahia na kutengeneza mkwanja ipo mikononi mwako unasubiri nini?

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA SASA

Acha ujumbe