Benjamin Sesko amefichua sababu zilizomfanya achague kujiunga na Manchester United, licha ya mvutano mkali wa usajili uliokuwa ukihusu jina lake. Jumamosi asubuhi, United ilithibitisha rasmi kumchukua Sesko kutoka RB Leipzig kwa dau linaloweza kufikia pauni milioni 74.
Awali, Arsenal ilionyesha nia ya kumsajili mshambuliaji huyo wa Kislovenia mapema majira haya ya joto, kabla ya kuamua kumsajili Viktor Gyokeres kwa ada nafuu zaidi. Newcastle, kwa upande wao, walitoa ofa kubwa kuliko ya United, lakini Sesko alikataa na badala yake kuchagua mpango wa kuhamia Old Trafford.
Akiweka wazi uamuzi wake, Sesko alisema kuwa haikuwa tu historia ya Manchester United iliyomvutia, bali zaidi ni maono ya baadaye ya klabu hiyo. “Historia ya Manchester United bila shaka ni ya kipekee, lakini kinachonipa hamasa zaidi ni mustakabali wake,” alisema Sesko. “Tulipojadili mradi wa klabu, ilikuwa wazi kila kitu kiko tayari ili timu hii iendelee kukua na kushindania mataji makubwa tena hivi karibuni.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
“Tangu nilipowasili, nilihisi mara moja hali chanya na mazingira ya kifamilia ambayo klabu imeyajenga. Ni sehemu kamili kwa mimi kufikia kiwango changu cha juu kabisa na kutimiza malengo yangu yote. Siwezi kusubiri kuanza kujifunza kutoka kwa Ruben Amorim na kuungana na wachezaji wenzangu ili kufanikisha mafanikio ambayo tunajua tunaweza kuyapata kwa pamoja,” aliongeza.
Usajili huu unaongeza nguvu kubwa kwenye safu ya ushambuliaji ya United, huku mashabiki wakisubiri kuona namna nyota huyu mpya atakavyong’ara katika msimu ujao.