Hali Ya Rodri Tia Maji Tia Mafuta Man City

Kiungo wa Klabu ya Manchester City, Rodri anaendelea kuuguza majeraha aliyoyapata kwenye mchezo wa kombe la Dunia la vilabu huku ikipambana kuhakikisha anakua sawa kuelekea msimu mpya wa ligi kuu Uingereza. Kiungo huyu wa kati alikosa sehemu kubwa ya msimu wa 2024/25 baada ya kupata jeraha kubwa la kuvunjika kwa ligamenti ya mbele ya goti mwezi Septemba mwaka jana. 

Hali Ya Rodri Tia Maji Tia Mafuta Man City

Majeraha hayo yalikuja wakati ambao Manchester City wanategemea mshindi huyo wa Ballon d’Or 2024 kusaidia kuirejesha timu yao kwenye kiwango cha juu katika ligi ya England baada ya msimu mgumu uliopita.

Hata hivyo, Guardiola amefichua kuwa Rodri alipata jeraha jingine katika mchezo wa mtoano wa robo fainali dhidi ya Al-Hilal, uliofanyika Marekani. “Rodri anaendelea kuimarika, lakini alipata jeraha kubwa katika mchezo wa mwisho dhidi ya Al-Hilal,” alisema Guardiola. 

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Hali Ya Rodri Tia Maji Tia Mafuta Man City

“Ameonyesha maendeleo mazuri katika mazoezi ya siku za hivi karibuni. Tunategemea baada ya mapumziko ya kimataifa atakuwa katika hali nzuri ya kucheza. Katika mechi hizi, anaweza kupata dakika za kucheza, lakini jambo muhimu ni asije akajitonesha ili tusije tukampoteza tena kwa majeraha. Tutajitahidi sana kuhakikisha anarejea salama. Ameanza kufanya mazoezi pamoja nasi kwa kipindi cha hivi karibuni, na hilo ni jambo la kupongeza.”

Iwapo hali hiyo itaendelea, basi Rodri atakosa mechi tatu za mwanzo za Premier League msimu huu. Manchester City wanatarajia kuanza kampeni zao kwa kucheza dhidi ya Wolves ugenini, kisha kucheza nyumbani dhidi ya Tottenham kabla ya kwenda kucheza na Brighton. Kwa upande wa timu ya taifa ya Hispania, Rodri atakuwa na nafasi ya kucheza katika mechi mbili za kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya Bulgaria na Uturuki mwanzoni mwa mwezi Septemba.

Hali Ya Rodri Tia Maji Tia Mafuta Man City

Kwa sasa, mshindi huyo wa Ballon d’Or anahitajika kupona kikamilifu ili kuweza kuendelea kutoa mchango wake mkubwa kwa klabu na taifa katika mashindano yanayokuja.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.