Simba : Hukumu ya Aveva, Kaburu Octoba 6.

 

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu inatarajia kutoa hukumu ya kesi inayomkabili Rais wa zamani wa Club ya Simba SC, Evans Aveva na wenzake Oktoba 6 mwaka huu ambapo itakua ni siku moja baada ya Mawakili wa pande zote mbili katika kesi hiyo kuwasilisha hoja zao za mwisho kama Washitakiwa wana hatia au la.

Mbali na Aveva Washitakiwa wengine katika kesi hiyo ni Godfrey Nyange (Kaburu) ambaye alikuwa Makamu pamoja na aliyekuwa Mwenyekiti wa kamati ya usajili Zachariah Hans Pope ambaye kwa sasa ni Marehemu.

Awali, Mahakama hiyo iliwaona Washitakiwa hao wanakesi ya kujibu katika mashitaka nane kati ya tisa yaliyokuwa yakiwakabili ambapo ni pamoja na kula njama, kughushi, kuwasilisha nyaraka za kughushi na kutoa maelezo ya uongo.

Katika shitaka la kughushi linalowakabili Washitakiwa wote inadaiwa walighushi hati ya malipo ya kibiashara ya Mei 28, 2016 wakionyesha kwamba nyasi bandia zilizonunuliwa na Simba SC zina thamani ya dola 40,577 sawa na zaidi ya Sh milioni 90 huku wakijua sio kweli.

Pia katika mashitaka mengine inadaiwa Aveva, Nyange na Hans Poppe kati ya Machi 10 na Septemba 30 mwaka 2016 waliwasilisha nyaraka za uongo kuonyesha Simba SC imenunua nyasi bandia zenye thamani ya Dola za Kimarekani 40,577.


SPACE SPIN NA MERIDIANBET.

Ni Mabingwa pekee Meridianbet wanakupa nafasi ya kushinda zaidi na mchezo wa Space Spin katika kasino bomba za meridianbet. Ni wakati wa kufurahia na kutengeza mkwanja bila kuwaza.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA SASA

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.