Klabu ya Simba SC, imefanikiwa kupata ushindi wa bao moja katika mchezo wa kwanza wa robo fainali ya Michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Orlando Pirates katika dimba la Mkapa Stadium.

Mchezo ulikuwa wa kasi kila timu ikijilinda na kushambulia kwa zamu, Simba SC ilifanikiwa kuliandama lango la Orlando na kumiliki sehemu kubwa ya mchezo kwa kutengeneza nafasi kadhaa.

 

simba sc, Simba SC Yaanza na Ushindi Shirikisho., Meridianbet

Mlinzi wa kulia Shomari Kapombe aliiandikia Simba SC bao la kwanza kwa mkwaju wa penati dakika ya 68 baada ya Bernard Morrison kufanyiwa madhambi ndani ya 18.

Simba SC sasa wanahitaji ushindi au sare ya aina yoyote katika mchezo wa marudiano utakaofanyika nchini Afrika Kusini ili kufuzu hatua ya nusu fainali ya mashindano hayo.

Kocha wa Simba, Pablo amekiri kuwa hawakuwa na matokeo mazuri kwenye mechi za ugenini katika hatua ya makundi kwa hiyo wanapaswa kujipanga kulingana na ubora wa wapinzani.

“Michuano ya Afrika mara nyingi timu zinafanya vizuri nyumbani kama tulivyofanya. Tutajipanga kuelekea mchezo wa marudiano ugenini tunahitaji kufuzu nusu fainali,” amesema Pablo.


VUNA MKWANJA NA AVIATOR

Maana halisi ya ushindi mkubwa unaipata katika kasino ya mtandaoni ya Aviator kutoka meridianbettz. Andaa kapu la ushindi wa mkwanja na beti kibao za BUREEE.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

SOMA ZAIDI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa