Baada ya mambo kuwaendea vibaya Ligi ya Europa dhidi ya Eintracht Frankfurt, kelekea mwisho wa msimu, kuna hisia kuwa Barcelona wanaweza kuikamata Real Madrid kwenye ligi.

Kwenye mkutano na waandishi wa habari kabla ya mechi kwa ajili ya mechi ijayo ya Barcelona na Cadiz, Xavi aliulizwa jinsi anavyoendelea kurejesha timu kwenye fomu.

“Ni kwa kuwapa motisha na kuwafanya wachezaji wafahamu kile ambacho hatufanyi vizuri. Tuko kwenye njia sahihi, lakini matokeo yanapaswa kupatikana.”

Barcelona wamekuwa wakiimarika, wakiwa na mechi 15 walizocheza bila kufungwa kwenye La Liga na kuwatoa Galatasaray na Napoli kwenye Ligi ya Europa.

Kwa mara nyingine tena, mapambano yao ya Ulaya yalirudi kuwaandama. Sport iliripoti mawazo ya Xavi kuhusu suala hilo.

“Kurejesha mtindo wa mchezo ambao ulipotea kunahitaji muda. Tunahitaji kujifunza kutokana na makosa yetu. Imepita miaka mitano tangu tufanye vyema Ulaya.”

Hatimaye, meneja aliulizwa ni nini hasa Barcelona ilihitaji kuboresha. Akisisitiza kuwa wanahitaji ushindi, hivyo wanahitaji kuongeza umakini kuanzia mwanzoni mwa mechi.


 

VUNA MKWANJA NA AVIATOR

Maana halisi ya ushindi mkubwa unaipata katika kasino ya mtandaoni ya Aviator kutoka meridianbettz. Andaa kapu la ushindi wa mkwanja na beti kibao za BUREEE.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

SOMA ZAIDI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa