Kiungo wa Tottenham, Moussa Sissoko amekamilisha usajili wa kuelekea Watford iliyopanda daraja msimu huu kwa mkataba wa miaka miwili.

Sissoko alisajiliwa Tottenham akitokea Newcastle siku ya tarehe ya mwisho mnamo Agosti 2016 na kucheza zaidi mechi zaidi ya 200 kwa klabu.
Sissoko alicheza kwenye Euro 2020 akiwa na Ufaransa. Akiwa amebakiza miaka miwili kwenye mkataba wake na Tottenham Hotspur lakini hayupo katika mipango ya meneja wa sasa Nuno Espirito Santo.
Bosi wa Watford Xisco Munoz alisema mapema Ijumaa: “Ni mchezaji mzuri sana, kila mtu anajua yeye ni mchezaji mzoefu.
“Ni mchezaji bora na nadhani atakuwa mzuri kwetu. Tutaona akifika. Daima tunasema kitu kimoja – tutakuwa na chaguo moja zaidi katika kikosi chetu kujaribu kuongeza ubora kwa timu yetu . “
Kuondoka kwake kunaashiria hatua nyingine katika ujenzi wa Tottenham baada ya kuondoka kwa Danny Rose, Erik Lamela na Toby Alderweireld.
Unawezaje kuikosa hii! Ndani ya kasino za meridianbet kuna mchezo unaoweza kukupa mkwanja mrefu leo hii, Wild Hot 40 ni njia nyingine ya kukufanya milionea, Chagua namba yako na uvune mkwanja.



Sarah
Sissoko Yuko vizuri