Meneja wa Klabu ya Manchester United, Ole Gunnar Solskjaer ameulizia uwezekano wa kumpata kiungo wa WolvesHampton Ruben Neves raia wa Ureno kama mbadala endapo watamkosa Declan Rice wa West Ham.

Solskjaer amekuwa akivutiwa na huduma ya Rice kutoka West ham lakini uwezekano wa kumnasa mchezaji huyo raia wa uingereza imekuwa kibarua kizito baada ya West Wam kuhitaji dau la kuanzia £80m -£100m.
Klabu ya Wolves imeripotiwa iko tayari kumuuza Neves majira haya ya kiangazi endapo klabu yoyote itafika dau la £35M ambalo linaweza kufikiwa na Manchester United.
Liverpool na Arsenal pia wamekuwa wakihusishwa na kiungo huyo wa Wolves kulingana na taarifa mbalimbali nchini uingereza. Bado hakuna timu iliyopeleka ofa official mpaka sasa.
Kasino ya Mayan Eagle inakukufanya kuwa bingwa wakati wowote unapoamua kuicheza. Utaburudika huku ukiendelea kutengeza mkwanja mrefu, jiunge sasa na uwe miongoni mwa mabingwa!!



Ernest
Man U wanatapatapa