Aliyekuwa kocha wa muda wa Tottenham Cristian Stellini ameondoka katika klabu hiyo kufuatia kichapo cha mabao 6-1 Jumapili dhidi ya Newcastle wakiwa ugenini.

Muitaliano huyo alikuwa ameteuliwa hadi mwisho wa msimu baada ya kuondoka kwa Antonio Conte mwezi uliopita, huku Ryan Mason akisaidia majukumu ya kikosi cha kwanza.
Lakini Stellini, ambaye hapo awali alikuwa kocha nambari 2 wa Conte, sasa ameacha nafasi yake baada ya mechi nne pekee, huku kiungo wa zamani Mason akisimamia mechi sita zilizosalia za Ligi Kuu ya klabu hiyo.
Katika taarifa iliyopatikana kwenye tovuti ya klabu, mwenyekiti Daniel Levy alisema: “Uchezaji wa Jumapili dhidi ya Newcastle haukubaliki kabisa ilisikitisha kuona matokeo hayo tunaweza kuangalia sababu nyingi kwa nini ilitokea na wakati mimi, bodi, makocha na wachezaji lazima tuchukue jukumu la pamoja, hatimaye jukumu ni langu.”

Cristian aliingia katika wakati mgumu katika msimu wetu na ninataka kumshukuru kwa njia ya kitaalamu ambayo yeye na timu yake ya makocha wamejiendesha katika wakati mgumu kama huu. Tunamtakia heri yeye na wafanyakazi wake. Ryan Mason atachukua majukumu ya ukocha mara moja kwani anaijua klabu na wachezaji vyema. Rais wa klabu hiyo alisema.
Pia aliongeza kuwa amekutana na kamati ya wachezaji jana na kikosi kimedhamiria kufanya kazi pamoja ili kuhakikisha kumaliza kwa nguvu zaidi msimu huu.
Wakati wa utawala wa muda mfupi wa Stellini, Spurs pia walitoka sare ya 1-1 na Everton, wakailaza Brighton na kufungwa 3-2 na Bournemouth, na kuwaacha Wana London Kaskazini kwa pointi sita kwenye mbio za nne-bora.

Mason mwenye miaka 31, atatarajia kuwachangamsha wachezaji wake kwa ziara ya Manchester United Alhamisi usiku, kabla ya safari ya kuelekea Anfield kumenyana na Liverpool siku ya Jumapili.

