Klabu ya Yanga ambayo ipo chini ya kocha Nasredine Nabi imetua Dar kibabe kutoka Nigeria baada ya kumtungua Rivers United mabao 2-0 katika hatua ya robo fainali ya kombe la shirikisho.
Yanga baada ya kuwa kinara wa kundi kwenye michuano hiyo hatua ya makundi alipangiwa Rivers ambayo walishawahi kukutana kwenye klabu bingwa na kumtoa baada ya kumpasua nje ndani sasa ilikuwa ni wakati wa kulipiza kisasi.
Mabao hayo amwili ya kuitanguliza Yanga mguu mmoja hatua ya Nusu Fainali ya Kombe hili yalitupiwa kimyani na Fiston Kalala Mayele huku akipokea pasi nzuri za mabao kutoka kwa Bakari Mwamnyeto.
Baada ya ushindi huo mnono sasa wananchi wametua asubuhi hii jijini Dar es salaam kwaajili ya kujiandaa na mchezo wa pili wa marudiano ambao utapigwa siku ya Jumapili katika Dimba la Benjamin Mkapa.
Hapa mwenye faida ni Young Africans ambaye tayari ana mtaji wa mabao mawili kazi kubwa inabaki kwa mgeni Rivers ambaye ana mlima wa kuupanda. Je ataweza kufanya nini akiwa ugenini? Unampa nafasi gani Mwananchi kutinga nusu fainali. ODDS KUBWA unazipata Meridianbet.