Yanga Yaibamiza Rivers Kwao

Klabu ya Yanga imefanikiwa kupata ushindi mbele ya Rivers United ya nchini Nigeria wakiwa ugenini kwenye mchezo wa hatua ya robo fainali wa kombe la shirikisho barani Afrika.

Klabu ya Yanga imefanikia kushinda kwa mabao mawili kwa bila kitu ambacho kinawapa faida kubwa kwenye mchezo wa marudiano ambapo utapigwa katika dimba la Benjamin Mkapa wiki inayofuata hivo na kwenda kwenye mchezo huo wakiwa na faida ya mabao mawili.YangaWananchi walionekana kuanza nyuma kipindi cha kwanza wakiwasoma wapinzani wao klabu ya Rivers United ambayo ilionekana kushambulia zaidi, Lakini licha ya kucheza nyuma vijana wa kocha Nabi walitengeneza nafasi lakini hawakuzitumia ipasavyo na kuweza kuwapa faida.

Kipindi cha pili Yanga walionekana kubadilika na kuanza kucheza zaidi wakioneakana kutafuta matokeo baada ya kutengeneza nafasi na mpaka kufikia dakika ya 73 ambapo Fiston Mayele aliweka bao la kuongoza na dakika ya 81 akipigilia msumari wa moto kwa kufunga bao la pili.YangaYanga msimu huu wameonekana kucheza vizuri sana kwenye michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika kwani hata kwenye makundi walifanikiwa kuongoza kundi mbele ya US Monastil ya nchini Tunisia, Hivo ni wazi klabu hiyo imedhamiria kufanya makubwa msimu huu kwenye michuano hiyo.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.