Garnacho Arejea Mazoezini Man United

Kinda wa klabu ya Manchester United Alejandro Garnacho ameonekana kurejea mazoezi kwenye klabu hiyo baada kupata majeraha yaliyomuweka nje kwa wiki kadhaa klabuni hapo.

Garnacho alionekana akiwa ameanza mazoezi ya peke yake kwenye gym ya klabu hiyo na kuonesha tayari anaweza kurudi uwanjani siku za karibuni, Mchezaji huyo alipata majeraha katika mchezo wa ligi kuu ya Uingereza dhidi ya klabu ya Southampton ambapo mchezo hu ulimalizika kwa sare.GarnachoWinga huyo wa kimataifa wa Argentina amekua na msimu mzuri ndani ya klabu ya Manchester United na kumfanya kocha Erik Ten Hag kumpa nafasi mara kwa mara, Hivo kukosekana kwake ndani ya wiki kadhaa ndani ya timu hiyo imeonesha pengo kwa klabu hiyo.

Baada ya Garnacho kuonekana akijifua mwenyewe imeibua matumaini kwa mashabiki wa klabu ya Manchester United kwani klabu hiyo imeandamwa na majeraha, Kwani wachezaji wake kadhaa wamepata majeraha na wengine kukosekana kwa msimu wote uliomalzika.GarnachoAlejandro Garnacho anaweza kurejea uwanjani siku za karibuni kuimarisha timu hiyo ambayo tayari imeshakumbana na majeraha ya wachezaji wawili ambao watakua nje kwa msimu mzima uliobakia, Hivo kurejea kwa klabu hiyo ni taarifa nzuri kwa klabu hiyo katika kuhakiksha wanamaliza msimu vizuri.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.