Taarifa zinaeleza kiungo wa klabu ya Real Madrid raia wa kimataifa wa Ufaransa Eduardo Camavinga anaandaliwa mkataba mpya ndani ya klabu hiyo ambao atausaini siku chache zijazo.
Camavinga atasaini mkataba mpya ndani ya Real Madrid huku maslahi yake ya mshahara yakiboreshwa zaidi tofauti na sasa, Mkataba wa mchezaji huyo bado ni mrefu ndani ya timu hiyo kwani mkataba ambao alisaini awali alipojiunga na timu hiyo mwaka 2021 unaisha mwaka 2027.
Lengo la klabu ya Real Madrid kumuongezea mkataba mrefu zaidi kiungo huyo wa kimataifa wa Ufarannsa inaelezwa ni taarifa za kuhitajika na vilabu mbalimbali kutoka nchini Uingereza, Hivo klabvu hiyo inataka kumfunga na kuweka kifungu cha kumuachia kwa kiwango kikubwa cha pesa.
Taarifa zinaeleza Camavinga mwenyewe anavutiwa zaidi kuendelea kuitumikia miamba hiyo ya soka kutoka nchini Hispania, Licha ya kuhusishwa na timu mbalimbali kutoka ligi kuu ya Uingereza ambazo zimekua zikifukuzia huduma ya kiungo huyo wa zamani wa klabu ya Stade de Rennes ya nchini Ufaransa.
Eduardo Camavinga amekua moja ya wachezaji muhimu sana kwenye kikosi cha mwalimu Carlo Ancelotti msimu huu kwenye kikosi cha Real Madrid mpaka sasa, kwani mchezaji huyo amekua kiraka akitumika kwenye maeneo tofauti tofauti kiwanjani na kufanya vizuri kiungo huyo amekua akitumika kama kiungo au beki wa kushoto na sehemu zote hizo anaonesha uwezo.

