Kiungo wa klabu ya Real Madrid na timu ya taifa ya Ufaransa Eduardo Camavinga amemsifu kiungo mwenzake wa klabu ya Real Madrid Luca Modric.
Kiungo huyo amefunguka kua Modrid anamsaidia vitu vingi sana tangu ametua ndani ya klabu hiyo mwaka 2021 akitokea klabu ya Stade de Rennes inayoshiriki ligi kuu ya soka nchini Ufaransa.
Camavinga tangu amejiunga na klabu hiyo amekua akitumika mara kadhaa kwenye kikosi cha mwalimu Carlo Ancelotti huku muda mwingi akiwa anatokea benchi kuchukua nafasi za wakongwe kama Modric na Toni Kroos.
Kiungo huyo wa kifaransa anasema Modric amemsaidia vitu vingi sana ikiwemo namna ya kua mtulivu na mpira, Na ni jambo kubwa na zuri kwake kukaa pamoja na mkongwe huyo kutokana na ubora wake na kujifunza vingi kupitia yeye.
Camavinga pia alitania kwenye mazungumzo yake na kusema Modric humtaka amuite baba kwakua kiungo huyo amepishana na Modric kwa takribani miaka 17. Hivo ni wazi kua mchezaji huyo angeweza kua baba yake.

Je wewe hucheza Kasino Mtandaoni na umekuwa ukijiuliza ni mchezo gani rahisi na mzuri kwa ushindi? Basi Usihangaike Aviator ni rahisi zaidi kucheza na kushinda, kingine cha zaidi ni kwamba Aviator Bonanza imerudi tena Cheza zaidi ujiweke kwenye nafasi ya kushinda Samsung A23.

