Kocha wa klabu ya Manchester United Erik Ten Hag amegoma kuzungumzia mambo binafsi kumhusu winga wake Jadon Sancho ambaye alikaa nje ya uwanja kwa kipindi kirefu.
Kocha Ten Hag wakati anazungumza na wanahabari aliulizwa ni nini haswa kilimfanya mchezaji wake Jadon Sancho kukaaa nje ya uwanja kwa kipindi kirefu na kusema “Nafikiri ni mambo binafsi na ninatakiwa kuheshimu hilo” Hii ilikua kauli ya kocha huyo.
Inaelezwa kua nyota Jadon Sancho licha ya majeraha yaliyokua yanamsumbua lakini mchezaji huyo alikua anasumbuliwa zaidi na mambo yake ya nje ya uwanja ambayo inasemekana yaliharibu saikolojia yake na kushindwa kuitumikia klabu yake.
Baada ya Sancho kupitia kipindi kigumu kutokana na mambo ambayo yalikua yanamsumbua nje ya uwanja, Kocha Erik Ten Hag aliweza kumpa mapumziko na kumuandalia programu maalumu ambayo ingeweza kurejesha utimamu wake wa mwili na akili ili aweze kua fiti kuitumikia klabu ya Manchester United.
Baada ya mchezaji Jadon Sancho kuingia kwenye programu maalumu ambayo ilimuwezesha kurudi kwenye utimamu wake na kuanza kuichezea klabu hiyo, Kocha Ten Hag amesema anafurahishwa na ujio wa kiungo huyo na anaamini ataongeza kitu kwenye eneo lao la mbele kwani ni mchezaji mwenye uwezo mkubwa.

