Kocha Jose Mourinho wa Tottenham Hotspur amesema sasa ameanza kuamini ukubwa wa uwezo wa Tanguy Ndombele baada ya Mfaransa huyo kufunga bao la dakika ya mwisho lililowasaidia kuwaondoa Lokomotiv Plovdiv ya Bulgaria kwenye Europa League.
Tottenham waliponea chupuchupu kuenguliwa mapema kwenye kipute hicho kilichoshuhudia Lokomotiv ya Bulgaria wakisalia kutegemea wachezaji tisa pekee baada ya Lima Almeida na Birsent Karagaren kuonyeshwa kadi nyekundu katika dakika za 78 na 79 mtawalia.

Georgi Minchev aliwaweka Lokomotiv Plovdiv kifua mbele kunako dakika ya 72 kabla ya Harry Kane kusawazisha mambo katika dakika ya 80 na Ndombele kufunga bao la ushindi dakika tano kabla ya kipenga cha kuashiria mwisho wa mechi kupulizwa.
Ndombele, 22, alisajiliwa na Tottenham kutoka Olympique Lyon ya Ufaransa kwa kima cha Sh7.5 bilioni mnamo Agosti 2019. Tangu wakati huo, sogora huyo alikuwa amewajibishwa katika mechi 17 pekee kwenye mashindano yote ya msimu wa 2019-20 kutokana na wepesi wa kupata majeraha na kushtumiwa na kocha Mourinho.
“Tanguy anaanza kuimarika. Nimeanza sasa kuamini uwezo wake,” akasema Mourinho ambaye mnamo Machi 2020, alitaka kiungo huyo “kujituma zaidi”.

“Ushawishi wake uwanjani haukuonekana kabisa msimu jana. Lakini kwa sasa amejitambua na anajitahidi sana hata mazoezini. Amepona jeraha na bao alilofunga litampa msukumo zaidi wa kupatamatokeo ya kuridhisha,” akasema.
Kutokana na ushindi wa Tottenham, Mourinho kwa sasa anajiandaa kuongoza kikosi chake kuvaana na Shkendija ya Macedonia mnamo Alhamisi ya Septemba 24 katika mechi ya raundi ya tatu ya mchujo wa Europa League.
Kabla ya hapo, Tottenham watapepetana na Southampton kwenye Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) mnamo Septemba 20 kisha kuchuana na Leyton Orient katika mchezo wa EFL Cup mnamo Septemba 22, 2020.

Iwapo wataibuka washindi wa mechi mbili za EFL na Europa League, basi Tottenham watasakata tena michuano mitatu chini ya siku saba wiki inayofuatia baada ya Septemba 27, 2020.
SHINDA NA MERIDIANBET!
Tengeneza pesa kidijitali kwa kubashiri mbio za farasi hapa Meridianbet! Chagua nani ashinde, unakusanya mkwanja.


Lydia Emmanuel Magoti
Mtanange watarii huo
Amiri Kayera
Nafax ya Tottenham kosonga mbele
Mariam mtandama
Habari njema
Shani
Tottenham wapambane wawez kurudi kwenye hadh yake
Fatina mfigi
Mmmh patakuwa hapatoshi
magdalena
spurs nina imani watakuwa wamejipanga vyema
Mwajumah
Mh kazi itakuwepo apo mana mtanange utakua wa atari huo#Meridianbettz
Nasra
Hapatoshi
Adelta
Tottenham Yuko vizuri@meridianbettz
Tatu
Leo apatoshi
Sauda
Tottenham ushindi
Gabriel
Tottenham Hotspur ndo nafas yao nzur kuongeza point wakijisahau watashuka
Caroline
Mambo ni motoo
Dorophina
Mda wao Tottenham kufanya maajabu ili kujipatia point waweze kusonga mbele zaid
felister
mourihno kwa sasa inabidi apambane ili aweze kushinda
Elika
Leo hapatoshi
Ernest
Ki ukweli Mourinho bado anakazi kubwa sana kukijenga kikosi cha Spurs ingawa tayari tunaona Spurs wanawachezaji wazuri sana
Rehema
Habari njema
Antony Luseno
Kwa kikosi cha spurs sio cha kutoa sare au kufungwa
Hopemwaikuka
Kaz kazin
Sadick
Ndombele ni mchezaji mzuri tatizo hakuwa anapata muda wa kutosha wa kucheza#meridianbettz
Hidaya
Tottenham wakaze wasikubali kushuka kiwango
Angelina
Kazi ipo
Tumaini kasalile
Kivumbi cha sika
Zeiyana
Mda wake mourinho wakufukia makosa yake
Mwanahamisi
Leo hapatoshi
aisha
Tottenham kazi wanayo inabidi wapambane sana
Khadija
Utakuwa mtanange wa kufa mtu#meridianbettz
Issa
Totenham inabid wafanye vizur kwakuw ni
Mashindano hayo makubwa yaliyobak kwaoi
Samiah
Leo patamu
Saupha mohamed
Kazi ipoo
Sabrina
Itakua hatarii
farida ahmadi
Safi Sana
Fatuma kasomo
Habar njm
Povel
Spurs inabid wapambane kwl msimu huu
Janeflora malisa
🔥
Asia Abdy
👏👏
Neema
Patanogaaa hatare
Latifa juma mohamed
Patanoga.
David Pere
Tanguy anaanza kuimarika. Nimeanza sasa kuamini uwezo wake,” akasema Mourinho ambaye mnamo Machi 2020, alitaka kiungo huyo “kujituma zaidi”.
Fatina mfigi
Itakuwa powah
warda
safi sana