Mchezo wa kwanza wa NBA Western Conference umeanza kwa matokeo ya ushindi wa LA Lakers dhidi ya Denver Nuggets.
Nuggets walianza vizuri mchezo huo kabla ya Lakers kubadilisha upepo kwenye kipindi cha pili. Mchezo wa kwanza umemalizika kwa Lakers kushinda kwa pointi 126-114.
Anthony Davis alikuwa mchezaji nyota kwenye mchezo huo baada ya kuipatia Lakers pointi 37 na kucheza mipira 10 iliyokufa.
“Tulichukua robo saa kubadili matokeo. Sisemi kwamba tumeshaumaliza mchezo huu, bado ni mapema sana kusema hivyo.” amesema mchezaji wa Lakers – LeBron James.
James aliisaidia Lakers kupata pointi 15, alitoa pasi 12 za magoli na kucheza mipira 6 iliyokufa.
Hii ni fainali ya kwanza kwa Lakers kwenye michezo ya Conferences tangu mwaka 2010. Mchezo wa pili utachezwa siku ya Jumatatu.
SHINDA NA MERIDIANBET!
Tengeneza pesa kidijitali kwa kubashiri mbio za farasi hapa Meridianbet! Chagua nani ashinde, unakusanya mkwanja.


Amiri Kayera
Mechi ilikua tafu Sana Ila Lakers daima ni washind