Tuchel : Nimefurahishwa na Kiwango cha Kepa.

 

Meneja wa Chelsea, Thomas Tuchel amesema amefurahishwa na kiwango alichoonyesha kipa wake namba mbili, Kepa Arrizabalaga katika mchezo wa robo fainali ya Carabao Cup dhidi ya Brentford.

 

Goli la kwanza la kujifunga la Pontus Jonsson liliwapa Chelsea uongozi katika dakika ya 80 ya mchezo kabla ya Jorginho kuongeza goli la pili kwa mkwaju wa penati katika dakika ya 85.

“Nimefurahishwa sana na kiwango kilichoonyeshwa na Kepa,” alisema Tuchel baada ya mchezo.

“Sijashangazwa kwasababu yupo hivyo, katika akili ya mtu na mwanamichezo anayewajibika kwasababu hicho ndicho anachokiweza zaidi na hichi ndicho anachofanya kila siku mazoezini na amepata matokeo yake.

“Naamini hiyo ni sababu kubwa ya kuwa katika kiwango hichi. Nina furaha sana. Tunamuhitaji katika kiwango hichi.” aliongeza Tuchel.

Kepa amecheza katika mizunguko yote mitatu ya kombe la EFL mpaka sasa, wakati Kipa namba moja Eduard Mendy akiwa chaguo la kwanza katika mechi za ligi.


KUWA BINGWA MSIMU HUU WA SIKUKUU NA OCEAN CALL

Nani hapendi kuwa bingwa na kujishindia mkwanja wa kusahato kuelekea katika sikukuu wiki hii. Mchezo wa Ocean Call kutoka kasino maridhawa za meridianbettz unakupa kila sababu ya kuifanya siku kuu yako kuwa ya kuvutia zaidi.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.