Aubameyang, Upo Sokoni Au Tukuvumilie?

Aliyekuwa nahodha wa klabu ya Arsenal, Pierre-Emerick Aubameyang, sasa ni mchezaji aliyetengwa miongoni mwa wachezaji wanaozingatiwa na Mikel Arteta.

Aubameyang amekuwa ni headline ya The Gunners kwa muda. Mazila yake yalianza mwishoni mwa msimu uliopita wakati ambapo kulikua na sintofahamu ya mkataba mpya, baadae mambo yalieweka, Pierre akasaini mkataba mpya wenye mshahara mnono.

Ukipeleka picha mbele, 2021/22 hii hapa, mshambuliaji huyu hana makali ambayo mashabiki wa Arsenal wamekuwa wakimuhusu nayo, kiwango duni uwanjani, mfumo wa maisha nje ya uwanja na namna anavyojiweka miongoni mwa wachezaji wenzake, vimekua changamoto kwa Mikel Arteta.

Ni mpole usoni lakini, silaha yake ni kwenye kufanya maamuzi. Mikel Arteta hajapoteza muda, ameamua kumvua unahodha Aubameyang pamoja na kumuondoa kwenye mipango yake uwanjani mpaka baada ya mashindano ya AFCON, Februari 2022. Hii inamaana kuwa, mchezaji huyo hategemewi kucheza mchezo wowote wa The Gunners mpaka mwakani.

Aubameyang

Uamuzi huu unazua mijadala mingi. Je, ni muda sahihi kwa Arsenal kumuweka sokoni nyota wao? Kilichotokea kwa Mesut Ozil, kinajirudia kwa Pierre? Pierre anatakiwa kujishusha na kuomba radhi kwa utovu wa nidhamu? Vipi kuhusu hatma ya washambuliaji wa Arsenal, wakati huu ambao Lacazzete na Nketiah wanamaliza mikataba msimu huu na hakuna anayeonesha kusaini kandarasi mpya?

Arteta anakumbwa na nini kule Emirate Stadium, anachokitaka ndio kinachokua au kuna kirusi kinaitembelea timu yake hasa katika idara ya ushambuliaji?


KUWA BINGWA MSIMU HUU WA SIKUKUU NA OCEAN CALL

Nani hapendi kuwa bingwa na kujishindia mkwanja wa kusahato kuelekea katika sikukuu wiki hii. Mchezo wa Ocean Call kutoka kasino maridhawa za meridianbettz unakupa kila sababu ya kuifanya siku kuu yako kuwa ya kuvutia zaidi.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.