Pambano la uzito wa juu wa WBC kati ya bondia wa uingereza Tyson Fury uzito dhidi ya Dillian Whyte hatimaye limethibitishwa.

Promota wa Fury anayeishi Uingereza Frank Warren alishinda zabuni ya juu zaidi katika historia ya masumbwi Ijumaa jioni, £31m yake ($41,025,000) akimpita Matchroom Boxing £24m ($32,222,222).
Whyte sasa atawania taji la dunia kwa mara ya kwanza katika maisha yake ya masumbwi dhidi ya Fury ambaye hajapoteza pambano, aliibuka na ushindi mnono mara mbili katika michezo mitatu ya kihistoria dhidi ya Deontay Wilder.
Sasa inatarajiwa Anthony Joshua atarudiana na Oleksandr Usyk kuwania mataji ya IBF, WBA na WBO.
Fury alipost Instagram muda mfupi baada ya kutangazwa kuwa pambano la WBC dhidi ya Whyte litafanyika nchini Uingereza, maneno “BIG GK IS COMING HOME, UK BABY” na kuambatanisha na mashairi ya wimbo ‘Three Lions’.
Dakika tano pekee zinakutosha kuwa mmoja wa washindi wa mkwanja mrefu ndani ya kasino pendwa ya meridianbettz katika sloti maridhawa ya KENO, moja ya michezo inayoipa thamani dau lako.


