West Bromwich Albion wameafikiana na Benfica na kurefusha mkataba wa kiungo Filip Krovinovic, 25, kwa mwaka mmoja zaidi.
Mwanasoka huyo mzawa wa Croatia alihudumu kambini mwa West Brom kwa mkopo mwingine wa mwaka mmoja msimu uliopita wa 2019-20.
Katika kipindi hicho, aliwajibishwa mara 40 na akafunga mabao matatu. Alichangia sana ufanisi wa kupandishwa ngazi kwa hadi Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) msimu huu.

“Najua maamuzi ya kusalia West Brom hayakuwa mepesi. Ndipo mchakato mzima ukawa mrefu kiasi hicho. Hata hivyo, ni fahari tele kuendelea kuchezea kikosi hiki ambacho kimeonyesha imani kubwa kwangu,” akasema.
“Nilimweleza kaka yangu kwamba hii hatua ya kurefusha muda wa kuchezea West Bromwich ni sawa na kurejea shuleni baada ya likizo ndefu nyumbani. Kisha unakutana upya na marafiki zako na kuelezana mambo mengi,” akasema Krovinovic.
West Brom wameanza msimu wao mpya katika EPL kwa kupokea vichapo viwili na kuambulia sare ya 3-3 dhidi ya Chelsea uwanjani The Hawthorns licha ya kuongoza mechi hiyo kwa 3-0 kufikia mwisho wa kipindi cha kwanza.

Walipata ushindi wa 3-0 dhidi ya Harrogate Town kwenye raundi ya pili ya Carabao Cup kabla ya kufungwa 5-2 na Everton katika mchezo wa EPL mnamo Septemba 19 uwanjani Goodison Park.
Baada ya kufungwa 3-0 na Leicester City katika mechi ya kwanza ya EPL msimu huu, West Brom waliondolewa na Brentford kwenye raundi ya tatu ya Carabao Cup kwa mabao 5-4 kupitia penalti. Mechi hiyo iliikamilika kwa sare ya 2-2 mwishoni mwa dakika 90.
Beti kwa Kitochi Kushinda 300,000,000!
Unajua kuwa unaweza kushinda milioni mia tatu kwa buku tu? Ndiyo! Unaweza kushinda kwa kupiga *149*10# na kubashiri. Ingia mchezoni!


magdalena
kijana ana mchango mkubwa sana katika timu ndo maana wameamua kumbakiza ili aendelee kuwaonesha maajabu yake
Adelta
Hii iko Vizuri kwa sababu kijana Yuko vizuri na anajuwa vyema anachokifanya
Rehema
Good
Elika
Safi sana kijana kijana yuko vizur
Dorophina
Habari njema kwa mashabiki zake maana anaujua mpira vizuri sana
Angelina
Goodnews
Mwajumah
Safi sana
Fatina mfigi
Mashabiki tunapenda habar nzur kma hizi!
Caroline
Safi sana
Venerose
Habari njema
Lydia Emmanuel Magoti
Vizuri
Tatu
Bora filip abaki hapohapo west hamu apige kazi anaweza akapata timu kubwa zaid
Ester jackson
Good
Khadija
Habari njema
Ernest
Deal zuri kwa Filip Krovinovic
Neema
Safi sana
Salma ngende
Vizuri
aisha
Bonge la dili kwa filip
Nasra
Hili dili
Sabrina
Sio mbaya
Venerose
Safi sana
Saupha mohamed
Safi
Rose kapinga
Wameiona kazi nzuri anayofanya
Hidaya
Habari njema
felister
dili zuri la kwa filipe
Sylvester
Filip Krovinovic atawasaidia sana Westb kama alivyowapandisha daraja
Amiri Kayera
Safi san kwa kumuongeaz
David Pere
West Brom wameanza msimu wao mpya katika EPL kwa kupokea vichapo viwili na kuambulia sare ya 3-3 dhidi ya Chelsea uwanjani The Hawthorns licha ya kuongoza mechi hiyo kwa 3-0 kufikia mwisho wa kipindi cha kwanza.
Sauda
Kijana yupo vizuri
Zeiyana
West brom wameona humuimu wa Filip na ndio maana wameamua kumbakisha clabuni hapo
Hopemwaikuka
Aina mbaya
Shani
Saf kwa West brom
Povel
Kila la kheri
Latifa juma mohamed
Deal Safi.
Gabriel
Deal zuri kwa Filip
Samiah
Safi