Klabu ya Yanga inajiaandaa na safari ya kuelekea nchini Morocco kwaajili ya mchezo wao wa hatua ya Mkaundi dhidi ya FAR Rabat huku mwamuzi wa mchezo huo akiwa ni Tom Ambongile.

Mchezo huo wa Kundi B wa Yanga dhidi ya FAR Rabat utapigwa Februari 7, 2026 huku timu zote zikiwa na hamu ya kupata matokeo ili kujiweka sawa kwenye msimamo wa kundi hilo kwenye Ligi ya Mabingwa.
Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limemteua Abongile (34) kuchezesha mechi hiyo ikiwa ni ya pili kwake kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu baada ya ile baina ya Esperance na Stade Malien.
Timu za Kaskazini mwa Afrika ambako lugha kuu inayozungumzwa ni Kiarabu, zimekuwa na bahati kubwa ya kutopoteza nyumbani pindi Abongile anapochezesha mechi.
Meridianbet inakwambia kuwa endelea kubashiri hapa kwani ODDS KUBWA na machaguo zaidi ya 1000 yapo hapa. Ingia kwenye akaunti yako na uanze safari yako ya ushindi sasa.
Mchezo baina ya Esperance na Stade Malien ambao amechezesha mwaka huu, ulimalizika kwa sare ya bila kufungana.
Msimu uliopita, refa huyo alichezesha mechi nne za mashindano ya Klabu Afrika ambazo zilichezwa Kaskazini mwa Afrika na wenyeji waliibuka na ushindi pasipo kuruhusu nyavu zao kutikiswa.
Abongile kiujumla amechezesha idadi ya michezo 12 ya Ligi ya Mabingwa Afrika ambayo ametoa idadi ya kadi 57 za njano na kadi moja nyekundu.

