Miamba ya Soka Nchini Misri, Zamalek wametishia kujiondoa kwenye Ligi Kuu ya Misri ikiwa wapinzani wao, Al Ahly hawatacheza michezo yao iliyoahirishwa.

Msimu wa Ligi Kuu ya Misri 2020-2021 ulianza mnamo Disemba 2020, ambayo ni tarehe ya kuchelewa isiyo ya kawaida ikizingatiwa kuwa msimu ligi huwa unaanza Septemba. Lakini, walilazika kufanya hivyo kwa sababu msimu uliopita ulisitishwa kwa zaidi ya miezi minne kwa sababu ya mlipuko wa Covid-19.

Mpango wa Shirikisho la Soka Misri “EFA” ulikuwa umepanga kumaliza msimu Septemba 30 ikiwa mambo yataenda kama yalivyo kwa Wawakilishi wao katika michuano ya Kimataifa.

Al Ahly na Pyramids zina michezo mkononi iliyoahirishwa kwenye ligi kwani bado wanashiriki mashindano ya Afrika na wanatarajiwa kucheza hatua za nusu fainali za Ligi ya Mabingwa na Kombe la Shirikisho ambazo zitachezwa kati ya Juni na Julai.

Kwa kuongezea, timu nyingine nyingi zitapoteza wachezaji wao muhimu ambao watashiriki kwenye Olimpiki ya Tokyo 2021; Hii inamaanisha kuwa michezo zaidi itaahirishwa kwa miezi mitatu ijayo.

Zamalek, ambao sasa wanakaa juu ya msimamo wa ligi na michezo sita zaidi ya walio nafasi ya pili Al Ahly, wanasema kwamba sio haki kwao kuendelea kucheza wakati wapinzani wao wanaendelea kuahirishiwa michezo yao.

Katika taarifa rasmi, Zamalek The White Knights wamepanga kwamba hawatoweza kucheza tena michezo ya ligi, baada ya wa mkutano wao na bodi ya EFA na wawakilishi wengine wa vilabu vya Ligi Kuu ya Misri.


MAANA KAMILI YA USHINDI KATIKA KASINO ZA MERIDIANBETI NI PAMOJA NA MCHEZO WA PANDA PANDA.

Hii ndiyo burudani yenye ushindi! Ingia kwenye kasino ya Meridianbet kufukuzia ushindi huu. Cheza sasa Panda Panda na uwe moja ya washindi na Mabingwa.

Gomes, Gomes : Sitafanya Usajili wa Kutisha., Meridianbet

CHEZA HAPA

ONI MOJA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa