Singida Big Stars Watimkia Rwanda

UONGOZI wa Singida Big Stars umeweka wazi kuwa umepewa mualiko na Klabu ya Rayon Sports ya Rwanda kwa ajili ya mchezo wa kirafiki ikiwa ni maandalizi ya mechi zao za ligi kwa msimu wa 2022/23.

Septemba 2,2022 kikosi cha Singida United kinatarajiwa kuelekea nchini Rwanda ambapo wamealikwa kwa mchezo wa kirafiki dhidi ya Rayon Sports.

Ofisa Habari wa Singida Big Stars Hussein Massanza amesema kuwa wachezaji wote wataondoka kuelekea nchini Rwanda.

“Tutaondoka na wachezaji wote ambao tumewasajili kwa ajili ya mchezo wetu wa kirafiki dhidi ya Rayon Sports utakaochezwa Uwanja wa Nyamirambo.

“Msafara huo utajumuisha benchi la ufundi pamoja na baadhi ya viongozi na mchezo wetu unatarajiwa kuchezwa Septemba 4 huku gharama zote zitagharamiwa na wenyeji wetu,” amesema Massanza.

Miongoni mwa nyota wa kikosi hicho watakaoibukia Rwanda ni pamoja na Pascal Wawa, Deus Kaseke, Metacha Mnata.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.