Ten Hag: "Antony Atacheza Dhidi ya Arsenal".

Erik ten Hag amesema Antony atafanya mazoezi na wachezaji wenzake wapya kwa mara ya kwanza leo, baada ya kukamilisha uhamisho wake kwenda Manchester United siku ya Alhamisi.

Erik Ten Hag

Mbrazil huyo alikuwa mmoja wa wachezaji wawili walioongezwa siku za mwisho kwenye kikosi cha Mholanzi huyo, akijiunga pamoja na Martin Dubravka aliyesajiliwa kwa mkopo kutoka Newcastle United.

Ten Hag: "Antony Atacheza Dhidi ya Arsenal".
Antony Akisaini Mkataba na Man Utd

Antony alitazama mechi yao dhidi ya Leicester City akiwa nyumbani kwani mechi hiyo ilikuja mapema sana kwake, lakini Ten Hag hajapuuza uwezekano wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 kucheza mechi yake ya kwanza dhidi ya Arsenal katika uwanja wa Old Trafford Jumapili.

Ten Hag: "Antony Atacheza Dhidi ya Arsenal".
Mshambuliaji wa Man Utd-Antony

Kocha huyo amethibitisha kuwa winga huyo anatazamiwa kushiriki katika kikao cha timu Ijumaa alasiri huko Carrington, na kisha atafikiria kama mchezaji huyo wa zamani wa Ajax yuko tayari kujumuishwa kwenye kikosi.

Ten Hag: "Antony Atacheza Dhidi ya Arsenal".

“Kesho (Ijumaa), tuna kikao cha timu na Jumamosi tuna kikao cha timu, kwa hivyo nitafikiria kisha tutachukua uamuzi.”

Ten Hag: "Antony Atacheza Dhidi ya Arsenal".

Erik amekuwa na muendelezo mzuri wa kupata matokeo baada ya ushindi kwenye mechi 3 mfululizo huku mechi inayofuata huenda ikawa ni ngumu kwake kulingana na mpinzani wake anayekutana nae kuwa na mwanzo mzuri kwenye msimu kwa kushinda mechi zote 5 walizocheza.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.