Golikipa namba moja wa timu ya Aston Villa Emiliano Martinez amesema kuwa amekuwa akikosa usingizi kutokana na jinsi ambavyo wameanza vibaya msimu huu wa ligi kuu. Alikiambia chombo cha habari cha michezo Uingereza.

Emiliano amekiri kuanza kwao vibaya kwa msimu wa ligi kuu ya Uingereza kunamfanya anakosa usingizi. Anasema hata wakishinda na akiruhusu goli, hakulala kabisa walipofungwa na Arsenal, anapata shida kupata usingizi.
Anapitia wakati mgumu wanapopoteza mchezo hiyo yote ni kutokana na mapenzi aliyonayo na klabu hiyo hivyo basi hukaza buti kwani hujisikia vibaya kuona watoto wakiwa wamevaa jezi ya klabu yake huku wakimuimba jina lake hapo ndipo humfanya aipende klabu hiyo na asalie hapo, huku akikosa usingizi.
Ameongezea kwa kusema kuwa wachezaji wanatakiwa kuwajibika kwa hali hiyo ya sasa na sio kocha wa timu hiyo Steven Gerad.
Emiliano na timu yake mpaka sasa wamepokea vichapo vinne kikiwepo kile cha mwisho walichopokea katikati ya wiki kutoka kwa vinara wa ligi Arsenal, ambapo walipoteza kwa mabao 2-1 kitu ambacho kimewafanya wawe chini kabisa ya msimamo ambapo wapo nafasi ya 19 kutokana na matokeo hayo.

Leo hii watakuwa nyumbani kuwaalika vijana wa Guardiola Manchester City ambao wapo nafasi ya pili kwenye msimamo na wamekuwa bora sana hasa katika eneno la ushambuliaji kwani ndio timu inayoongoza kwa kufunga mabao mengi mpaka sasa. Matokeo ambayo wanayapata Aston Villa hayo yanaweza kusababisha kocha wao kibarua chake kuota nyasi.

