Kelvin De Bruyne kiungo mshambuliaji wa Manchester City huenda akaifikia rekodi ya mshambuliaji wa zamani wa Liverpool Steven Gerrard mwenye asisti 92 kwenye Ligi kuu ya Uingereza kwa muda aliocheza.
- Gerrard ana assist 92 za Ligi kuu
- De Bruyne akipumua shingoni akiwa na 89
- Giggs anashikilia rekodi ya muda wote akiwa na Assist 162

Nahodha namba mbili wa Manchester City amejidhihirisha kuwa mmoja wa wachezaji bora wa muda wote katika miaka saba aliyokaa Etihad. Katika mechi 215, amefanikiwa kupiga pasi za mabao 89 akiwa kabakiza Assist 3 ili kufikia Assist 92 za Gerrard alizotoa wakati wa maisha yake ya Ligi Kuu akiwa Liverpool.

Kabla ya kukutana na Aston Villa, Guardiola alisema: “Samahani kwa Steven Gerrard lakini rekodi yake ya [assist] itavunjwa, mapema au baadaye. Nina hakika Gerrard atafurahi ikiwa mtu ambaye atashinda rekodi yake mchezaji kama Kevin.

“Nadhani anatoa mifano mizuri kwa vizazi [vijavyo] na watoto wakati wote wa jinsi ya kuwa mchezaji wa mpira na jinsi ya kuishi, bila mitandao ya kijamii, maisha rahisi. Kisha kama mchezaji, yeye ni wa kipekee hivyo anaweza fanya chochote anachotaka na natumai anaweza kudumisha kiwango hiki kwa muda mrefu.”
De Bruyne ana asisti nyingine 74 ili kuvunja rekodi ya muda wote ya Ryan Giggs (162) ya Ligi kuu. Winga huyo wa zamani wa Manchester United yuko kwenye dunia yake katika suala hilo na Mbelgiji huyo ndiye mchezaji pekee anayeweza kuvuka rekodi yake kwa sasa.

Thierry Henry anashikilia rekodi ya kutoa pasi nyingi zaidi za mabao katika msimu wa Ligi Kuu ya Uingereza. Alipiga pasi 20 za mabao wakati wa msimu wa 2002-03 na pia kufunga mabao 24 katika moja ya rekodi za kipekee za muda wote.

NINI KINAFUATA KWA DE BRUYNE? Assists nne zaidi zitamfanya De Bruyne kumpita Gerrard na kuwa nafasi ya saba kwenye orodha ya asisti za Ligi kuu. Kisha atakuwa na David Silva (93) na Dennis Bergkamp (94) mbele yake.

