Timu ya Manchester City iliondolewa kwenye michuano ya Ligi ya Mabigwa Ulaya baada ya kukubali kipigo cha 3-1 katika uwanja Santago Bernabeu siku ya Jumatano.

Manchester City Yafungashwa Vilago Ligi ya Mabingwa

City ambao ndiyo viongozi wa Ligi kuu ya Uingereza walikuwa wanaongoza kwa 1-0 muda wote wa mchezo mpaka Rodrygo alipofunga katika dakika ya 90 bao la kusawazisha na kuongeza bao pili hali iliyopepelekea mchezo uende dakika 120 baada ya aggregate kuwa ni 5-5

Bao la tatu lilifugwa na Karim Benzema kwa mkwaju wa penati dakika ya 95 bao lililoipa tiketi ya kwenda Paris, ambapo finali ya mwaka huu itachezwa na sasa Real Madrid atamenyana na Liverpool kuwania taji la Ligi ya Mabingwa.

“Tulikuwa karibu. Tulikuwa karibu. Lakini mwisho hatukuweza kuifikia,” Guardiola aliambia BT Sport baada ya zawadi hiyo kuteleza kwenye vidole vyake tena.

“Waliweka wachezaji wengi kwenye eneo la hatari, Militao, Rodrygo, Vinicius, Benzema na waliweka krosi na kufunga mabao mawili.

VINJARI KASINO YA MTANDAONI HAPA UTENGENEZE PESA

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa