Kocha mkuu wa klabu ya Aston Villa Steven Gerad alalamikia maamuzi ambayo refa wa mchezo huyo ameyafanya baada ya kupuliza filimbi na kukataa goli lao ambalo Philipe Coutinho alifunga kitu ambacho kingefanya waondoke na alama tatu.

Gerad amesema hayo akihojiwa na Skysport baada ya kumalizika kwa mchezo wao waliokuwa wakicheza jana wamzunguko wa sita ambapo walikuwa wakimkaribisha Manchester City na mchezo huo kumalizika kwa sare ya 1-1.
Aston Villa mpaka sasa wameshinda mchezo mmoja tuu wa ligi kuu na wamepoteza michezo minne kitu ambacho kinawafanya wawe katika nafasi ya pili kushuka chini. Gerad anasema Goli ambalo lilifungwa na mchezaji wake lilikuwa goli halali kabisa huenda refa hakuwa sawa kwenye kutoa maamuzi.

Kwa usajili ambao wamefanya Villa unaweza kuongeza kitu katika timu yao na huenda wakikaa kwa muda wanaweza kuwa na muunganiko mzuri au wakicheza kwa kujituma na juhudi wanaweza wakamaliza katika nafasi nzuri msimu huu.

