Kocha mkuu wa timu ya Atletico Madrid Diego Simeone amesema kuwa anatumaini kuwa golikipa wake Jan Oblak anataepuka jeraha lolote baya ambalo amelipata kwenye mchezo wao dhidi ya Real Sociedad kitendo ambacho kilifanya atolewe nje ya mchezo, ambao uliomalizika kwa sare ya bao 1-1.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Slovenia alibadilishwa dakika ya 85 baada ya kugongana na Reinildo katika jaribio la kumzuia Umar Sadiq ambapo aliumia paja. Atletico watakuwa wakitoa jasho kutokana na utimamu wa Oblak lakini pia akiwa ni makamu nahodha kwa upande wakishinda Zamora Trophy ya Laliga wakishinda mara 5 ikiwemo 2020/2021 huku Oblak akiwa hajakosa hata mechi moja.
Simeone amesema kuwa anatumaini kuwa mlinda mlango huyo hatakaa nje na kusubiri majibu ya daktari kutokana na kuumia kwakwe. Simeone amekataa sare ambayo wameipata dhidi ya Real Sociedad baada ya goli lao lililofungwa na Alvaro Morata kukataliwa kwa mpira wa mkono ulioonekana wazi kwa Joao Felix, huku bao la Umar Sadiq la kusawazisha kwa Sociedad pia likitokea kwa mkono likisimama.
Hata hivyo meneja wa timu ya Atletico, Thomas Renones alikuwa muwazi zaidi kuhusu mwamuzi, akidai kuwa waamuzi walikuwa na siku mbaya sana. Lazima tuelewe kuwa waamuzi wanaweza kuwa na siku mbaya na leo ni mafano wa siku mbaya.

“Tumeona maamuzi tofauti. Waamuzi hutupatia mazungumzo kila mwaka mwanzoni na kisha kinachofanywa ni tofauti kabisa.”

