Jadon Sancho mchezaji wa klabu ya Manchester united na timu ya taifa ya Uingereza amefanikiwa kushinda tuzo ya goli bora la mwezi wa nane ndani ya klabu yake.
Goli lililoweza kushinda tuzo ni goli alilofunga katika mchezo dhidi ya mahasimu wao wakubwa klabu ya Liverpool mchezo uliopigwa katika dimba la Old Trafford wiki moja iliyopita.
Sancho amekua na kiwango kizuri msimu toka kwenye mechi za kujiandaa na ligi mpaka kuanza kwa ligi ikiwa tayari akiwa ameshafunga magoli mawili tayari msimu huu ndani ya klabu hiyo kwenye michezo ya ligi.
Sancho hakua na msimu mzuri kwenye msimu uliomalizika ikiwa ni tofauti na msimu huu ambapo inaonekana ameanza kurudisha uwezo wake taratibu ambao alikua akiuonesha katika klabu ya Borussia dortmund.
Kumekua na utaratibu wa klabu ya Manchester unite mashabiki kupiga kura na kuchagua mchezaji bora wa mwezi wa klabu pamoja na goli bora hivo kupitia njia hiyo goli la mchezaji lilipata kura nyingi na kushinda tuzo hiyo.

