Roberto Lewandowski mshambuliaji wa klabu ya Fc Barcelona ya nchini Hispania ameendelea kufunga kama anavyotaka ndani ya klabu yake hiyo mpya.
Lewandowski amefanikiwa kufunga magoli matano kwenye mechi nne alizocheza katika ligi kuu nchini Hispania maarufu kama La Liga hii inaonesha ni kwa kiasi gani nyota huyo ameendelea kuonesha dunia haikua bahati katika ligi kuu ya ujerumani na ana uwezo wa kufunga popote.
Mshambuliaji huyo wa zamani wa klabu ya Bayern Munich amefanikiwa kufunga michezo miwili mfululizo huku michezo miwili akifunga magoli kila mchezo kabla ya jana kufunga goli moja dhidi ya Sevilla na kufikisha idadi ya magoli matatu katika ushindi wa goli tatu kwa bila walioupata klabu ya Barcelona.
Lewandowski wakati anafikisha goli tano mpinzani wake kutoka klabu ya Real Madrid ambae ndio anashikilia kiatu hicho yeye akiwa ameweka kambani mabao matatu mpaka sasa kwenye michezo nne mbio za kiatu bado mbichi tusubiri kuona ni nani atafanikiwa kukitwaa kati ya washambuliaji hao hatari.

