Kocha wa Manchester City Pep Guardiola alilaumu kushindwa kwa wachezaji wake kufanya ‘mambo mepesi’ kwa kutoa sare ya 1-1 dhidi ya Aston Villa.
Villa ilitangulia kwa bao lingine kutoka kwa mchezaji mpya Erling Haaland muda mfupi baada ya kuanza kwa kipindi cha pili lakini Leon Bailey aliwasawazishia vijana wa Steven Gerrard baadaye.

Timu zote mbili zilipata nafasi ya kushinda mchezo huo, na akizungumza na BBC baada ya mchezo huo, Guardiola alikiri kwamba ilikuwa mbali na utendaji wao bora.
Alisema: “Ulikuwa mchezo mzuri, hatukuambulia chochote katika kipindi cha kwanza. Tulijitahidi kidogo kutengeneza nafasi lakini tulidhibitiwa kabisa.
“Kipindi cha pili tunavunja mchezo na tulikuwa bora zaidi. Tulikuwa tunajaribu kufunga bao la pili na tulifanya makosa ya kiulinzi wakasawazisha.

“Hatukuwa sahihi katika mchezo wetu wa tatu wa mwisho. Wachezaji wengi hawako sawa katika mambo rahisi na ndiyo maana wakati mwingine hii hutokea, lakini ni sawa, pointi moja tumepata na tunaendelea.
“Sisi ni wanadamu, sisi ni wachezaji wa mpira wa miguu na hii hutokea.”

Guardiola alikubali kwamba nafasi alizokosa zilikuja kuwaandama, akisema: “Erling Haaland alihusika kwenye mchezo, alikuwa na miguso na nafasi. Tulipata nafasi mbili au tatu nzuri katika kipindi cha kwanza na kipindi cha pili baada ya 1-0, aligonga nguzo kutoka kwa Kevin [de Bruyne] na akawa na mwingine kutoka kwa Kevin na mwingine kutoka kwa Phil [Foden].
“Kwa hiyo tulipata nafasi za kutosha kufunga la pili na la tatu na la nne. Lakini kwenye Epl, ukiwa 1-0 lolote linaweza kutokea. Hatukutetea hali hiyo moja na tukatoka sare.”

