Pep Guardiola ambae ni kocha wa klabu ya Manchester City mabingwa watetezi wa ligi kuu Uingereza ampa pole aliekua mchezaji wa Liverpool Steven Gerrard kwasasa kocha wa Aston Villa.
Guardiola amemuelelza nahodha huyo wa zamani wa Liverpool kua rekodi yake ya pasi za mabao inakwenda kuvunja na kiungo wa klabu ya Manchester City Kevin de Bruyne ambae amefikisha jumla ya pasi za mabao 89 huku Gerrard akiwa na pasi 92 huku gwiji huyo akimzidi idadi ya michezo kiungo huyo raia wa Ubelgiji alie kwenye ubora mkubwa.
Kevin de Bruyne amekua kwenye kiwango bora sana tangu arejee kwenye ligi hiyo akitokea nchini ujerumani kwenye klabu ya Wolfsburg ambapo alicheza kwa kiwango bora sana akitokea klabu ya Chelsea ambapo alionekana kufeli.
Pep anaamini kiungo wake huyo anakwenda kuvunja rekodi ya Gerrard kwani ana muda mrefu wa kucheza zaidi na pia ameachwa kwa idadi ndogo ya pasi za mabao 89 kwa 92 ikiwa ni namba chache haswa kwa mchezaji wa kariba ya De Bruyne.

