Renan Lodi asajiliwa na Nottingham Forest kwa dau la paundi milioni 30 na ada ya uhamisho ya paundi milioni 5 ambazo zitalipwa Atletico Madrid.

Beki wa pembeni wa klabu ya Atletico Madrid Renan Lodi atajiunga na klabu ya Nottingham Forest ya Uingereza kwa uhamisho wa thamani ya paundi Milioni 30.

Lodi Atua Nottingham Akitokea Atletico Madrid.
Renan Lodi Akiwa na Uzi wa Atletico Madrid

Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa mwandishi nguli kwa habari za usajili Fabrizio Romano ameandika kuwa tayari makubaliano baina ya timu mbili pamoja na makubaliano binafsi na Lodi yamekamilika.

Lodi Atua Nottingham Akitokea Atletico Madrid.
Lodi akiwa kwenye majukumu ya Timu ya Taifa la Brazil

Kinachosubiriwa hivi sasa ni Lodi kufanyiwa vipimo vya afya ya mwili na kusaini mkataba wake mpya, ambapo mpaka sasa beki huyo raia wa Brazil amesalia na mkataba wa miaka na Atletico Madrid.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa