Mats Hummels: Ampongeza Jude Bellingham.

Mats Hummels nahodha nahodha wa klabu ya Borussia Dortmund amempongeza kiungo wa klabu hiyo Jude Bellingham baada ya kufata nyayo za wachezaji Earling Haaland na Kylian Mbappe.mats hummelsMats Hummels amempongeza kiungo huyo baada ya kufunga kwenye mechi nne mfululizo za ligi ya mabingwa ulaya akiwa kwenye umri mdogo jambo ambalo wamelifanya kina Kylian Mbappe kwenye msimu wa 2017 na Earling Haaland kwenye msimu wa 2019.

Jude alifanikiwa kufunga katika mchezo wa jana ambao timu yake ilitanguliwa kwa bao moja na klabu ya Sevilla wakiwa nyumbani na Jude alifanikiwa kusawazisha bao hilo na kumfanya kufunga kwenye mechi nne mfululizo za ligi ya mabingwa barani ulaya msimu huu.

“Jude daima anataka kushinda kila mchezo. Anawekeza sana, Nafikiri wote tunampenda huyu kijana” Alisema Mats Hummels.mats hummelsJude Bellingham kijana mwenye miaka 19 tu ila anaonesha ubora mkubwa sana katika klabu yake ya Borussia Dortmund na kuanza kutabiriwa makubwa katika maisha yake ya mpira.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.