Kocha mkuu wa Tottenham Antonio Conte amekiri kuwa timu yake lazima ifanye vyema katika kukabiliana na mechi kubwa baada ya kupoteza hapo jana kwa mabao 2-0 walipokuwa ugenini kucheza mchezo wake wa 11 dhidi ya Manchester United.

Mabao hayo ya vijana wa Ten Hag yalipachikwa na Fred pamoja na Bruno Fernandez na kupata pointi 3 wakiwa nyumbani huku ikiwa ni mara ya pili kwa Conte kupoteza mechi toka msimu uanze kwenye Primia Ligi baada ya kutandikwa na vinara wa EPL Arsenal.
Spurs wameanza vyema ligi na bado wanashikilia nafasi ya tatu kwenye msimamo kwa pointi sawa na Manchester City ambapo wapo nafasi ya pili ingawa Spurs wapo mbele mchezo mmoja.
Antonio Conte almezungumza kuhusu suala la usajili wa dirisha kubwa na kusema kuwa United walifanya matumizi makubwa ya pesa kwenye kusajili wachezaji kama kina Casemiro, Martinez na Antony na kuwaleta Uingereza hapo ambao waaonekana wana mchango kwenye timu yao.

Spurs pia walitumia pesa kuwanunua Yves Bissouma, Djed Spence na Richarlison miongoni mwa wengine, lakini Mbrazil huyo hakuweza kucheza Old Trafford kutokana na jeraha.
“Ninaichukulia United kuwa timu nzuri sana,” Conte alisema. “Unajua vyema uwezo wa klabu hii, walichokifanya kwenye soko la uhamisho na pesa wanazoweza kutumia, Kwa hakika tunazungumza kuhusu viwango viwili tofauti.
Hakuishia hapo alisema kuwa pia katika aina hiyo ya mchezo wanaweza kufanya vizuri pia ambapo walijitahidi na kupambana dhidi ya Chelsea, dhidi ya Arsenal na hapo jana walijitahidi.

Masheatani wekundu walistahili kushinda, walicheza mchezo mzuri sana na kwa upande wao kwenye huo mchezo walitakiwa kuwa na kiwango cha juu na walihitajika kuimarika zaidi pia alisema kuwa wanapaswa kujaribu kuwa bora zaidi ya jana.

