Staa wa klabu ya Manchester United Cristiano Ronaldo amezua gumzo baada ya kuondoka kabla ya mchezo kumalizika dhidi ya Tottenham katika dimba Old Trafford.
Staa huyo alionesha kukasirishwa na kitendo cha kutopata nafasi katika mchezo huo na kufikia hatua ya kuondoka uwanjani dakika ya 89 wakati klabu ya Man United ikiwa inaongoza goli mbili kwa bila na kupelekea kuzua gumzo kubwa klabuni hapo pamoja na mashabiki wa soka duniani.
Kitendo hicho alichofanya Ronaldo kimepokelewa kwa sura tofauti na watu tofauti wengine wakisema yupo sahihi na wengine wakikosoa na kuamini amekosa nidhamu kutokana na kitendo hicho alichofanya.
Wanaomtetea gwiji huyo wanaamini kocha wa klabu hiyo anamkosea heshima mchezaji huyo kutompa nafasi ya kucheza klabuni hapo huku wanaeamini kakosea wakisema staa huyo amekosea kwani mwalimu ndo ana haki ya kupanga timu anayoitaka kutokana na mahitaji ya mchezo hivo kama mwalimu aliamua Staa huyo ahatacheza alipaswa kuheshiu maamuzi ya mwalimu.
Baada ya mchezo huo kocha wa klabu hiyo Eric Ten Haag aliulizwa kuhusu Ronaldo na kitendo alichokifanya “Nitashugulika na jambo hilo kesho, Sio leo. Tunasherehekea ushinda kwasasa” kutokana na majibu ya mwalimu huyo inaonesha hajapendezwa na kitendo alichofanya staa huyo.
Hali hii inaogopwa kutokana na wataalamu wa mambo wanavyoeleza kua staa huyo anaweza kuigawa timu hiyo na kusababisha mkwaruzano kwenye timu hiyo.

