Man United Yaibamiza Tottenham Tena.

Klabu ya Man United imeendeleza ubabe dhidi ya klabu ya Tottenham jana usiku baada ya kuifunga klabu hiyo katika mchezo wa ligi kuu Uingereza uliopigwa katika dimba la Old Trafford.

Mchezo huo ambao United walifanikiwa kushinda mabao mawili kwa bila huku magoli ya klabu hiyo yakifungwa na Fred pamoja Bruno Fernandes ambaye alipiga msumari wa mwisho na kuifanya timu hiyo kuondoka na alama tatu muhimu.man unitedKlabu hiyo ya Tottenham imeendeleza uteja mbele ya mashetani wekundu jana baada ya kukubali kufungwa mechi ya tatu mfululizo hii ni baada ya msimu uliomalizika kufungwa michezo yote miwili waliyokutana katika ligi kuu ya Uingereza.

Klabu ya Man United baada ya kupata matokeo dhidi ya Tottenham imefanikiwa kufikisha alama 19 na kubakia nafasi ya tano ya msimamo wa ligi hiyo huku wakiwa na mchezo mmoja mkononi.man unitedKatika mchezo huo ambao mashetani wekundu walitawala mchezo huo muda mwingi wa mchezo na kufanikiwa kutengeneza nafasi nyingi zaidi ndani ya msimu huku kipa wa klabu ya Tottenham akiokoa mashuti kumi yaliyoelekea langoni kwake.

 

Man United wamekua kwenye kiwango sana bora katika mchezo wa jana huku mashabiki wa klabu hiyo wakiomba uwe mwendelezo kuelekea michezo mingine inayofuata.

Acha ujumbe