Anchelotti Kazi Yangu Ipo Salama.

kocha wa klabu ya Real Carlo Anchelotti amesema anafikiri kazi yake ipo salama baada ya kiungo wa klabu hiyo Federico Valverde akiendelea kufunga michezo katika klabu hiyo.

Kiungo huyo raia wa Uruguay ambaye amekua kwenye kiwango bora sana tangu kuanza kwa msimu huu na kumfanya kocha wa timu hiyo kuweka imani kubwa mchezaji huyo na kumtaka kumfunga magoli kumi na kumuahidi kama atashindwa basi ataachana na kazi ya ukocha klabuni hapo.anchelottiMpaka kufikia jana Federico Valverde amefanikiwa kufunga magoli 6 huku ikiwa ni mwanzo wa msimu hivo kumfanya kocha wa timu Anchelotti kuamini kiungo anaiweka kazi yake kwenye mikono salama.

Real Madrid ambao walikua ugenini jana dhidi ya Elche na kufanikiwa kushinda mabao matatu kwa bila huku Valverde nae akifunga katika mchezo huo.anchelotti“Valverde sio mtu wa kawaida! Naamini atafunga zaidi ya magoli kumi. Hivo kazi yangu ipo salama”Alisema Anchelotti huku akicheka.

Kocha Carlo ameonesha imani kubwa kwa Valverde na kiungo huyo mpaka wakati huu hajaonesha chembechembe yeyote ya kumuangusha kocha huyo.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.